Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Shirika la Mzinga Morogoro yamechuana vikali kwenye fainali za mchezo wa riadha katika michuano ya SHIMMUTA iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mashindano ya riadha yaliwavutia watazamaji wengi ambao walishuhudia ushindani wa hali ya juu kati ya wanariadha wa mashirika hayo mawili yenye historia ndefu katika michezo ya SHIMMUTA.