Timu ya Mpira wa Pete ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) imeirudisha darasani timu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kuichapa magoli 48 kwa 46 katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliofanyika Disemba 2, 2025.

Mchezo huo uliokuwa wa kusisimua uliwavutia mashabiki wengi waliofurika uwanjani kushuhudia ubingwa wa wachezaji wa vyuo hivyo viwili vikubwa nchini.