Michezo ya SHIMMUTA 2025 imefungwa kwa sherehe kubwa na ya kufana katika Uwanja wa Jamhuri jijini Morogoro, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima tarehe 06 Disemba 2025.

Washindi wa michezo mbalimbali walikabidhiwa vikombe na medali huku wakipongezwa kwa ushiriki na ari kubwa waliyoonyesha katika mashindano yote. Mwenyekiti wa SHIMMUTA aliwashukuru wadhamini, wachezaji na mashirika yote yaliyoshiriki.

Sherehe hiyo ilihitimisha wiki nzima ya mashindano yaliyokutanisha mashirika ya umma, taasisi na makampuni binafsi kutoka kila kona ya Tanzania.