SHIMMUTA inaungana na Watanzania wote, hususan wananchi wa Zanzibar, kuadhimisha miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Maadhimisho haya ni kumbukumbu ya ujasiri, umoja, usawa na mshikamano uliojenga misingi muhimu ya maendeleo ya Zanzibar na Taifa kwa ujumla. SHIMMUTA inathamini nafasi ya michezo katika kuimarisha afya, kuunganisha watu na kukuza upendo miongoni mwa wafanyakazi wa mashirika ya umma, taasisi na makampuni binafsi.

Tunawatakia wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.