SHIMMUTA inaungana na wanawake wote nchini na duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Tunatambua mchango mkubwa wa wanawake katika uongozi, michezo, maeneo ya kazi, familia na maendeleo ya Taifa. Kupitia michezo ya mashirika, SHIMMUTA inaendelea kuhamasisha ushiriki wa wanawake, kuimarisha afya na kujenga mazingira yanayotoa fursa sawa kwa wote.

Heri ya Siku ya Wanawake Duniani kwa wanawake wote.