Baadhi ya washindi wa michezo mbalimbali walikabidhiwa vikombe na medali kutoka kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima, wakati wa sherehe za ufungaji wa michezo ya SHIMMUTA katika Uwanja wa Jamhuri tarehe 06 Disemba 2025.

Zawadi hizo ni sehemu ya kutambua juhudi na ushindi wa timu na wanamichezo waliofanya vyema katika mashindano ya mwaka huu.