Wawakilishi wa makampuni na mashirika yaliyodhamini michezo ya SHIMMUTA walikabidhiwa zawadi za shukrani kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima tarehe 06 Disemba 2025.

SHIMMUTA imetambua mchango mkubwa wa wadhamini katika kufanikisha mashindano ya kila mwaka yanayokutanisha wafanyakazi wa Tanzania.