Kuelekea michezo ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) itakayofanyika jijini Mwanza, droo ya michezo hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 05 Novemba jijini Dar es Salaam katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Droo hiyo itapanga makundi na ratiba ya mashindano kwa mashirika yote yatakayoshiriki msimu ujao.