Smart Sports, Mdhamini Mkuu wa Mashindano ya SHIMMUTA 2025, imekabidhi vifaa vya michezo kwa uongozi wa SHIMMUTA.

Ukabidhi huo unaonyesha ushirikiano thabiti kati ya SHIMMUTA na wadau wake katika kuendeleza michezo ya wafanyakazi. Vifaa vya michezo vinasaidia kuongeza ubora wa mashindano, usalama wa washiriki na hamasa kwa taasisi zinazoshiriki.

SHIMMUTA inaendelea kuwashukuru wadhamini na washirika wote wanaowezesha michezo kuwa jukwaa la afya, umoja na ushindani wenye nidhamu.