Mwenyekiti wa SHIMMUTA, Bi. Roselyne Massam, amezungumzia maandalizi, ushiriki na mwenendo wa michezo ya SHIMMUTA.

Katika ujumbe wake, Mwenyekiti amesisitiza umuhimu wa ushirikiano, nidhamu, afya na maandalizi bora kwa taasisi zote zinazoshiriki. Ameendelea kuwashukuru wadau, wanamichezo na viongozi kwa mchango wao katika kukuza michezo ya wafanyakazi nchini.

SHIMMUTA itaendelea kuwa jukwaa la kuimarisha afya, mahusiano na mshikamano miongoni mwa wafanyakazi.